Like Us On Facebook

ROMA:NATAMANI MASHABIKI WA KIKE



ROMA Mkatoliki, Msanii wa Hip Hop Bongo, amesema kuwa amegundua kuwa, kila wakati anapotoa nafasi ya mashabiki wake wote kuchat naye na kumwuliza maswali yoyote kwa njia ya mtandao, kumekuwa na ushiriki mdogo sana wa watoto wa kike/ wanawake, Kitu ambacho ameona kuwa ni tatizo kwake kama msanii.

ROMA ama pia Baba Ivan kama anavyofahamika, amesema kuwa ugunduzi hu umempatia changamoto kuwa kwa sasa anatakiwa kujitahidi kufanya kitu kwaajili ya kuwavuta zaidi jinsia ya pili (them ladies) kwenye pool ya mashabiki wake.
Kutokana na sentensi hii kutoka kwa rapa huyu kuleta hisia kuwa huenda akabadilisha na kulegeza zaidi aina ya muziki anayofanya, Yeye binafsi amesema kuwa hana mpango wowote wa 'kulainisha' muziki wake, ila yupo katika mchakato wa kuufanya uwavutie zaidi warembo.... sooo stay tuned.
 



TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari