Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa.
ABIRIA
kadhaa akiwemo Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli, Mhe. Edward
Lowassa wamenusurika kifo, baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria
kupasuka matairi yote manne ya nyuma wakati ilipokuwa ikitua katika
uwanja wa ndege wa Arusha mchana mchana huu.
Ndege hiyo ya
shirika la ndege la Precision aina ya ATR ilipata ajali hiyo wakati
ikitua. Matairi yote manne ya nyuma yamepasuka na kusababisha taharuki
kubwa kwa abiria.
"Yaani Mungu ni mkubwa kwa kweli, ametunusuru maisha yetu na kiongozi kipenzi chetu Lowassa...Mungu atamlinda jamani...siamini" alisikika akisema mama mmoja miongoni mwa abiria hao wakati akishuka.
Lowassa ni miongoni mwa wana CCM wanaotajwa kuwania urais 2015 na amekuwa na nguvu kubwa katika harakati hizo.
SHUHUDA ANASEMAJE?
Nikiwa
mmoja wa abiria tuliosafiri na PW kurudi Arusha leo, ndege ya shirika
hilo yenye usajili No 5HPWI imepata kizaazaa wakati wa kutua baada ya
tairi mojawapo kupasuka kwa kishindo, likufuatiwa na mengine yote ya
nyuma ambapo yalipasuka pia na kuacha vipandevipande kwenye njia ya
kurukia.
Waliookota vipande hivyo wamesema kuwa wamekuta
viraka(pechi, watu wa magari wananielewa zaidi hapa), kitu ambacho si
kawaida kwenye usafiri wa jamii hii!
Rubani wa ndege hiyo
amejitahidi kuitoa ndege hiyo nje ya njia ili kutozuia ndege nyingine
kuruka, japokuwa mwishowe ilimgomea kabisa na kubaki ikisota pembeni mwa
njia hiyo.
Kikubwa ni kwamba hakuna madhara yaliyowapata abiria, akiwemo Bwana Lowassa.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.