Like Us On Facebook

Shilole aivaa laana ya mzee Small baada ya kumzushia kifo.

 
MSANII wa muziki wa mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuandika juu ya uzushi wa kifo cha msanii mkongwe,  Said Ngamba ‘Mzee Small’ kupitia mtandao wa Instargram.
 
Shilole ambaye baada ya kugundua kuwa hakuwa sahihi kuandika juu ya kifo hicho kwani haikuwa kweli, alilazimika kukanusha na ndipo akaanza kuporomoshewa ‘mvua’ ya matusi.

Baadhi ya maneno makali yaliyoandikwa mtandaoni humo kumtukana  Shilole, ambayo hayawezi kuandikika kwa kuzingatia maadili, yalimtaka kujiepusha na tabia ya kudandia na kueneza mambo pasipo kuyafanyia uchunguzi.

Mwandishi wetu alipomtafuta msanii huyo kuzungumzia juu ya suala hilo, alikiri kuandika juu ya kifo hicho huku akionesha majuto ya hali ya juu.
“Ni kweli niliandika maneno ya taarifa za kifo cha Mzee Small, japo nilikuwa nikiandika jinsi ambavyo msanii huyo amezushiwa kifo, sasa watu wakadhani mimi ndiye nimeandika kwa kujitungia, najuta sana kuchapisha ujumbe huo,” alisema Shilole.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari