Baada ya juzi kati kuripotiwa habari ya aliyekuwa producer ama
mtengenezaji wa vipindi vya Wema Sepetu Chidi Mohamed kufukuzwa kazi
kutokana na kulitumia gari la kampuni kama sehemu yake ya kuvunjia amri
ya sita na wadada wa mjini, hatimaye katika pitapita zetu za mtandaoni
tuliweza kukutana na kauli ya producer huyo akizungumzia habari hiyo ya
yeye kufukuzwa kazi kwenye kampuni ya Endless Fame ya wema sepetu.
Chidi mwenyewe anasema kuwa habari hizo si za kwel na ni kwamba
wote walioandika wamepanga kumchafua tuu kwa kuogopa kuwa anaweza
kuyaniika mambo mazito yanayoendelea huko endless Fame
Kwa mujibu wa chidi anasema kuwa yeye ameondoka kwenye Kampuni
hiyo siyo kwa sababu ya uzinzi ngani ya gari kama ilivyoripotiwa bali ni
kutokana na sababu hizi kuu mbili.
1. Ameona hamna jipya na wala hamna maendeleo yoyote ndani ya Kampuni hiyo ndio maana ameamua kuondoka
2. Wafanyakazi wa Endless Fame hawalipwi
kabisa ndio maana yeye akaamua kujitoa kwani anafanya kazi bure na pia
sio yeye peke yake aliyeondoka bali kuna wafanyakazi zaidi ya watatu
walioondoka kwenye kampuni hiyo ila nashangaa ni kwanini wameamua
kumchafua yeye?
Bado tunafanya mawasiliano na Endless Fame ili tujue kama daia haya ni ya kweli au la..Endelea kuwa na kilelechahabari BLOG.