Like Us On Facebook

NIGERIA,IVORY COAST ZA KWANZA KUKATA TIKETI YA BRAZIL 2014

HIZO ZINAKUWA FAINALI ZA TANO KWAO KUFUZU

TIMU ya taifa ya Nigeria imekuwa nchi ya kwanza ya Afrika kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani baada ya ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Ethiopia leo.

Victor Moses alifunga kwa penalti dakika ya 20 na Victor Obinna akaongeza la pili dakika ya 82 kwa mpira wa adhabu, hivyo Super Eagles kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-1, baada ya awali kushinda 2- mjini Addis Ababa mwezi uliopita katika mchezo wa kwanza.On the attack: Chelsea's Mikel John Obi takes the ball ahead of Ethiopia's Adane Girma (left) and Shemeles Bekele (right) during the match in Calabar
On the attack: Chelsea's Mikel John Obi takes the ball ahead of Ethiopia's Adane Girma (left) and Shemeles Bekele (right) during the match in Calabar
Hottest ticket in town: Supporters arrive for the second leg with a World Cup place at stake
Hottest ticket in town: Supporters arrive for the second leg with a World Cup place at stake

Nigeria inafuzu kwa mara ya tano kucheza Fainali za Kombe la Dunia, ambazo mwakani zitafanyika nchini Brazil, baada ya awali kucheza fainali nne zilizopita. Mechi nyingine nne za kufuzu kwa fainali hizo barani zitakamilika ndani ya siku nne wayi mchezo mwingine wa leo ni kati ya Senegal na Ivory Coast.

YAUNGANA NA NIGERIA KUWA TIMU MBILI ZA KWANZA KUFUZU FAINALI HIZO KUTOKA AFRIKA


Ivory Coast 

TIMU ya taifa ya Ivory Coast imefuzu Fainali zijazo za Kombe la Dunia baada ya sare ya 1-1 usiku huu ugenini na Senegal kwenye Uwanja wa Mohamed V in Casablanca, Morocco.

Matokeo hayo yanaifanya Didier Drogba na wenzake wafuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-2 na kuungana na Nigeria iliyoitoa kwa jumla ya mabao 4-1 Ethiopia. Ikiwa inajivunia ushindi wa 3-1 katika mchezo wa kwanza, Tembo walilazimika kusota kusawazisha bao baada ya Moussa Sow kutangulia kuwafungia Simba wa Teranga kwa penalti, kabla ya Salomon Kalou kusawazisha dakika za majeruhi. Kikosi cha Senegal: Coundoul, S. Sane, L. Sane, Mane, Badji/Saivet dk82, P. Cisse, Mbodji, Gueye, Souare, Djilobodji na Ndoye/Sow 66. Ivory Coast: Barry, K. Toure, Bamba, Gosso, Zokora, Romaric, Aurier, Y. Toure, Kalou, Gervinho/Sio dk80 na Drogba
 
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari