Kuna sababu zaidi ya 100 kuwa ‘ile inayoitwa’ movie ya Diamond na
Wema Sepetu iliyopewa jina na Diamond, ‘Temptations’ haipo na kama
unaingoja, utaingoja hadi miguu iingie tumboni. Hakuna movie.
Diamond
na Wema Sepetu walikuwa wakila bata na kufurahia kama wapenzi wengine
wanaopendana kwa dhati. Kwa kuangalia picha tu, ni rahisi mno kujua
penzi zito kati ya wawili hawa. Picha hizo ni ishara kuwa, Diamond na
Wema hawajawahi kuachana na Diamond amekuwa akimcheat mpenzi wake Penny.
Wazungu
wanasema, kama hujafanya utafiti hauna haki ya kuzungumza, hivyo ili
kuonesha kuwa hizi si brabra tu, tumefanya utafiti kwanza.
Wema, Diamond na binamu yake Romeo wakiwa Hong Kong
Ukweli
wa kwanza tulioubaini ni kuwa, Diamond na Wema Sepetu walikutana Hong
Kong na sio Malaysia. Wema alienda huko takriban wiki tatu zilizopita na
hivyo Diamond alimfuata baada ya kumaliza show yake ya Malaysia. Kwa
mujibu wa msichana aitwaye Alice aliyeiambia Bongo5, Diamond alisafiri
kutoka Kuala Lumpur, Malaysia kwenda Hong Kong kumfuata Wema kwa ndege
ya kampuni ya Air Asia.
“Nilipanda na Diamond flight moja from
KUL to HKG tena ilikua ni Air Asia X flight number 567 alipandia
KUL-LCC Terminal nilimuona kwenye lounge direct nikashangaa anafanya
nini huku na baada kufika HKG sijui hata alipotelea wapi kumbe haya yote
ndo alikua akiyafuata hongera zao,” alisema Alice.
Huko,
Diamond na Wema wamekaa wote kwenye hoteli moja na mpenzi wake Penny
hakuwa anajua kuhusu hili hadi picha hizi zilipoanza kuenea na yeye
ameshtuka kama walivyoshtuka wengine.
Haijajulikana picha hizo
zimesambazwa na nani lakini kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, kuna
uwezekano kuwa picha hizo zimesambazwa na Wema wenyewe kwa kusudi la
kumuumiza Penny. Kuna taarifa zimeifikia Bongo5 kuwa, Penny ameumizwa
mno na picha hizo na amekuwa akilia siku nzima. Hata hivyo binafsi
hatujaweza kuthibitisha taarifa hizo.
Jitihada za kumtafuta Penny azungumzie suala hili zimegonga mwamba kwakuwa simu yake haipokelewi.
Penny
Hivi
karibu kwenye birthday ya Diamond, Penny alielezea kuwa uhusiano wake
na Diamond ndio mgumu zaidi katika mahusiano yote aliyowahi kuwa nayo.
“Not
the easiest relationship I’ve ever had..but its the most intresting!
When I’m down, he would make me feel on top of the world, my bestfriend,
my brother, my soulmate, my baby, my man. My strength, my joy, my love,
Ohhh!!! What else do I gotta say? I love u, and its been a blessing to
have met you, u taught me that love is just Me&You the rest shouldnt
matter or make me loose my sleep, today I ask God to bless u a million
more times, the sweetest boyfriend ever!!! Crazie too..unpredictable
mind, through the ups and downs Im gona hold you down til God says
so..you have taught me that love conquers all, that Love is pain, but
the pain is worth the while..I love you baby,” aliandika Penny.
Miaka
ya nyuma, Wema na Penny walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa mujibu wao
wenyewe, urafiki wao uliharibika hata kabla ya wote kufahamiana na
Diamond.
“Urafiki hatuna,” Penny aliliambia jarida la Mzuka
kwenye makala ambayo haikuwa kutoka. “Mimi sidhani kama nina uadui naye
personally, sijui yeye na urafiki hatuna. Let me just say kwamba sio
kwasababu ya Diamond. Nadhani mimi na yeye tulikuwa tuna issue zetu
nyuma ambazo hazikuwa resolved so tulikuwa tuna distance mimi na yeye.
Tulikuwa hatuongei maybe kwa mwaka labda kama sio miezi nane, we had our
own issues kwahiyo hatukuwa marafiki vile tena kama tulivyokuwa zamani.
So mimi kuwa na uadui naye sidhani kama nina uadui. Mimi am happy
unajua, mimi ndo hivyo mimi naishi maisha yangu am happy na nilichonacho
am happy with my man, am happy na watu wangu so am good mimi sina
tatizo naye kabisa.”
Naye Wema kwenye interview na Mzuka aliwahi kuzungumzia alivyojiskia Diamond kuwa na uhusiano na Penny, rafiki yake wa zamani.
“It’s
a free world, kila mmoja ana uhuru wake wa kuishi anavyotaka yeye. They
met, they fall in love wameanza mapenzi, mtu yoyote anaweza kufall in
love na mtu yeyote asiwe questioned. Love doesn’t ask why, haiulizi
kwanini, because alikuwa rafiki yangu then I can’t NO. Wapendana, I wish
them all the best. Mimi na Penny si kwamba hatuongei sio sababu ya hii
issue, tuna drama zetu tu za huko nyuma kwahiyo hii issue ni muendelezo
tu,” alisema.
Ikumbukwe kuwa, Wema na Diamond waliwahi kuingia
kwenye ‘kile kilichoonekana’ kama ugomvi mzito, baada ya Diamond
kumrekodi mpenzi wake huyo wa zamani alipompigia na kuisambaza sauti
kwenye vyombo vya habari.
“Sikuwahi kudhani kwamba Naseeb ni
mtu wa aina hiyo kufanya kitu alichokifanya. Though nimesema kwamba
nitaacha kama ilivyo na nisingependa kuiongolea lakini nilikuwa very
disappointed, very very disappointed,” Wema aliliambia Mzuka.
Tunasubiria kushuhudia muendelezo wa drama hii kutoka kwa Malkia na Mfalme wa drama Tanzania.