KAMA kawaida yake, Rihanna amepiga picha kwa ajili ya jarida la GQ la Uingereza akiwa nusu utupu tangu juu hadi chini.
Mwimbaji huyo maarufu duniani amelipamba jalada la mbele la jarida
hilo toleo la Novemba akiwa hajavaa chochote cha maana tangu juu
ukiachilia mbali kichwa chake ambacho kimezingirwa na kufunikwa na
majoka.
Rihanna akiwa amefunikwa na majoka kichwani.
Picha hizo zimepigwa na Mariano Vivanco kwa kusimamiwa na Damien
Hirst, zikitoa taswira ya simulizi ya Kigiriki kuhusu Medusa (mlinzi wa
kike) ambayo imetumika katika kuadhimisha mwaka wa 25 wa jarida hilo.
Toleo hilo litakuwa mitaani tarehe 31 Oktoba mwaka huu.
Picha zote kwa hisani ya Akaunti ya Instagram ya Badgalriri.