|
Wema Sepetu akiwa katika hali ya majonzi baada ya kufiwa na baba yake mzazi |
|
Mama mzazi wa Wema akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe mzee Sepetu. |
|
Kajala
Masanja (kushoto), Wema Sepetu (katikati) na Zamaradi Mketema (kulia)
wakiwa katika hali ya majonzi nyumbani kwao Wema Sepetu, Sinza - Mori
jijini Dar. |
|
Kajala Masanja (kushoto) na Wema Sepetu (katikati) wakiangua vilio. Kulia Zamaradi akijaribu kumtuliza Wema. |
|
Ndugu wa karibu wa marehemu akiwa na simanzi nzito |
STAA wa sinema za Kibongo na Miss Tanzania 2006 Wema Isaac Sepetu,
bado yuko kwenye wakati mgumu baada ya leo asubuhi kupatwa na msiba
mkubwa wa kuondokewa na baba yake mzazi Balozi Isaac Abraham Sepetu
aliyefariki asubuhi ya leo.
Kwa sasa kuna watu wengi wamefika kumjulia hali maeneo ya Sinza, Mori
jijini Dar, rafiki yake wa karibu Kajala Masanja na Zamaradi Mketema
wapo bega kwa bega kuwa naye karibu na vilio vimetawala kila kona ya
familia ya marehemu Balozi Sepetu.
Bado haijafahamika mazishi yanafanyika lini maana wanasubuliwa watoto
wa Marehemu Tunnu Sepetu na Sunna Sepetu ambao wanaishi nchini
Marekani, lakini kuna tetesi kuwa huenda mazishi hayo yakafanyika siku
ya Ijumaa.
Mama mzazi wa Wema bado yuko kwenye hali ya huzuni baada ya kufiwa na
mume wake ambaye amedumu nae kwa miaka mingi kabla ya kupatwa na mauti
asubuhi ya leo katika hospitali ya TMJ jijini Dar. Mpaka mauti
yanamfika, marehemu alikuwa akisumbuliwa na kisukari pamoja na kiharusi.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.