Like Us On Facebook

Rais Kikwete apendekeza NYERERE DAY iwe siku aliyozaliwa na siyo siku aliyofariki dunia...Una Maoni gani juu ya hili?


             Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amependekeza kuwa siku ya ‘Nyerere day’ inayoadhimishwa October 14 kila mwaka, iadhimishwe siku aliyozaliwa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Rais kikwete ameyasema hayo alipokuwa akiwahutubia wananchi mjini Iringa katika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru, iliyoambatana na kumbukumbu ya baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.
 
Amesema anapendekeza siku hiyo iwe siku ya kuzaliwa ili watu washerehekee kwa furaha, wakikumbuka hotuba za Mwalimu.
 
Endapo mapendekezo ya rais yataungwa mkono, Nyerere day itakuwa  April 13, kwa kuwa mwalimu alizaliwa siku hiyo mwaka 1922.
Una  mtazamo  gani  juu  ya  pendekezo  hili?
-timesfm

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari