Anafahamika kama Snura
Mushi ni wanadada mwenye vipaji vingi ndani ya tasnia ya bongo movies.
Pamoja na kuwa mwigizaji aliyekuja kwa kasi sana pia Snura ni
mwanamuziki wa bongo fleva anayefanya vizuri sana sokoni kwa nyimbo zake
mbalimbali zenye mahadhi ya pwani mithili ya mduara. Pamoja na kuwa na
umbo na sura nzuri ya kuvutia snura pia amekuwa akitawala sana vichwa
vingi vya habari,magazeti na redio kutokana na uwezo wake mkubwa wa
kukata kiuno kwenye nyimbo zake.
Snura Mushi (Jina lake
halisi) alizaliwa tarehe kumi na mbili (12) mwezi wa kwanza (1) mwaka
1984 Jijini Dar es salaam ambako aliweza kukua na kupata elimu yake hapo
hapo Dar es salaam.
Kipaji cha mwanadada Snura Kiligunduliwa na mtu aliyefahamika kwa jina la Siasa. Ambaye ndiye aliyemfuata na kumshauri kuigiza baada ya kuvutiwa na uzuri na umbo lake ambalo kwa mujibu wa mtu huyo alikuwa na “star look” na angeweza kufanya vizuri kama angejiingiza katika sanaa. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2006. Na mwaka huo alipata nafasi ya kuigiza kwenye Filamu ya Mfalme Seuta iliyodirectiwa na Gumbo Kihorota. Baadaye aliweza kucheza movie za Zinduna na Hitimisho.
Snura alianza kujipatia umaarufu sana kupitia Filamu ya ITUNYAMA, na pia kupitia igizo la Jumba la dhahabu alizofanya akiwa chini ya director Tuesday Kihangala “Mr Chuzi”.
Akizungumzia maisha yake ya ustaa, Snura anasema kuwa huwa anaumizwa sana pale anapoona habari kwenye vyombo vya habari zinazomuhusu ambazo mara nyingi anasema huwa si za kweli.
Katika maisha yake ya kila siku Snura hupendelea sana kukaa ndani na kutazama Filamu mbalimbali kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali.