NYUMBA
anayoishi kiungo wa Yanga SC, Haruna Niyonzima, maeneo ya Magomeni
Makuti, Dar es Salaam imeungua moto usiku wa kuamkia leo na kusababisha
hasara ya vitu kadhaa.
Habari
zilizoifikia BIN ZUBEIRY zimesema kwamba nyumba hiyo anayopanga
mchezaji huyo wa kimataifa wa Rwanda, imeungua zaidi eneo la sebuleni na
fenicha zote, Teleisheni na Redio zimeteketea kwa moto.
Janga
hilo lilitokea wakati mchezaji mwenyewe akiwa ndani ya nyumba yake na
kama si jitihada za majirani kujitokeza kumsaidia kuzma moto huo, athari
zingekuwa kubwa.
Imeelezwa nyumba hiyo ina wapangaji wawili na upande ulioathirika kwa moto ni ambao anasihi mchezaji huyo tu.
Jitihada
za kumpata Haruna mwenyewe haraka kuzungumzia suala hilo hazijafanikiwa
na zinadenelea, wakati Ofisa Habari wa Yanga SC, Baraka Kizuguto
alisema amesikia taarifa hizo ila anasubiri kupata uhakika kamili kutoka
kwa mchezaji mwenyewe.
“Kweli ninawashukuru sana majirani kwa
kuonyesha uungwana wa hali ya juu, bila ya wao nyumba yote ingeungua.
CREDIT : SALEH JEMBE
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.