Wakaazi
wa mtaa wa kwanza wa Mathare Kaskazini nchini kenya walishuhudia kioja
cha mwaka pale maiti ilipogoma kusafirishwa jana usiku hadi eneo la
Kendu Bay kwenye kaunti ya Homabay. Maiti ya mwenda zake Peter Otieno
ilisafirishwa baadaye leo alasiri mishale ya saa tisa kasorobo baada ya
jamaa zake wa karibu kufanya mila na desturi ya jamii ya waluo ambapo
maiti ilibembelezwa na kubadilisha mwili wa marehemu kwenye jeneza ili
kichwa kilalie upande wa nyuma wa jeneza.
TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILO HAPA CHINI