Like Us On Facebook

INDIA YATATHMINI HASARA ILIYOSABABISHWA NA KIMBUNGA

Kimbunga Phailin kikipiga Orissa na Andhra Pardesh  
                Maafisa wa India wanaoshughulika na kazi za uokozi wameanza shughuli zao baada ya Kimbunga Phailin kupiga majimbo ya mashariki na kusababisha mafuriko kwenye miji na vijiji.

Wakuu wanasema wasaidizi wametumwa maeneo yaliyopigwa na kimbunga katika majimbo ya Orissa na Andhra Pardesh, kuwaokoa wale wanaofikiriwa wamenasa chini ya vifusi.

Miti iliyoporomoka imeua  watu wapatao saba ingawa waandishi wa habari wanasema matayarisho na operesheni kubwa iliyofanywa ya kuwahamisha watu kabla ya kimbunga, imenusuru maisha ya watu.

Kiwango cha uharibifu uliotokea bado hakijulikani kikamilifu ingawa waya za umeme na mawasiliano vimekatika katika maeneo mengi.

Kimbunga cha mwaka 1999 kiliuwa watu 10,000 katika jimbo la Orissa
 BBC Swahili
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari