

Ulinzi na ukaguzi katika Uwanja wa Taifa umekuwa ni mkubwa sana na zoezi hilo limeanza tangu Jumamosi iliyopita kwenye mechi ya Simba na Ruvu Shooting ambapo hakuna aliyeruhusiwa kupita bila kukaguliwa kwa kifaa maalum. Kufuatia mpango huo wengi walinaswa wakiwa na vitu wasivyostahili kuingia navyo uwanjani hapo.

Vilevile utaratibu mpya ulioanzishwa katika uwanja huo ni kutoruhusu mtu yeyote kuingia ndani ya uwanja na gari isipokuwa ya watu maalum tu.
MLIMANI CITY
Tofauti na hali ilivyokuwa siku chache nyuma, ulinzi wa sasa ‘si wa kitoto’ kwani mbali na magari kukaguliwa kwa umakini mkubwa, pia watu hupitishiwa kifaa maalum mwilini ambacho huweza kubaini uwepo wa silaha au kitu kingine cha hatari.

“Kweli sasa ulinzi unatisha kila kona ya nchi na hata kama hao magaidi wana mpango wa kuvamia Tanzania, watakuwa na kazi kubwa ya kufanya. Lakini hili suala la kuruhusu magari yenye namba za serikali yapite maeneo yenye mkusanyiko wa watu bila kukaguliwa siyo sawa,” alisema Hassan Maulid wa Kimara jijini Dar.

Kufuatia habari za kiuchunguzi ambazo zimekuwa zikiandikwa na magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers likiwemo hili la Risasi Mchanganyiko, wadau wametoa pongezi zao na kuomba juhudi ziendelee ili kuweka mambo kwenye mstari.
Picha kubwa iliyotumika ukurasa wa 16 ni ya mwanamke gaidi anayedaiwa kuongoza mashambulizi nchini Kenya, Samantha Lewthwaite ‘Mjane Mweupe’.