Kila mwanamke ana mvuto wake, wapo wanaojivunia nyuso zao zenye macho yaliyoumbwa yakaumbika, nyuso zisizo na chunusi wala aina yoyote ya kovu...
Wapo pia wanaojivunia makalio yao na sote tumekuwa tukishuhudia jitihada mbali mbali za akinadada za kujitengenezea makalio ya bandia ( ya kichina ) ili kujiongezea mvuto kwa wanaume.
Hali ni tofauti kidogo kwa msanii Ray C.Yeye anaamini kwamba mapaja ndo kila kitu na kwamba ni hicho kigezo muhimu kinachoangaliwa na wanaume wengi wa siku hizi...
"Nani asiyejua kwamba kuna makalio ya kichina? Umewahi sikia wapi mapaja ya kichina?..Haya tunayo wachache ambao tumejaliwa na muumba wetu".Hii ni kauli ya Ray C alipokuwa akipiga stori na mpekuzi wetu.
"Sitachoka kuwashukuru watanzania wenzangu ambao walikuwa pamoja nami pindi nikiwa mgonjwa. Nguvu zangu kwa sasa nimezielekeza katika kuiimarisha afya yangu na ndo maana unaniona niko hivi kwa sasa.
"Haikuwa kazi nyepesi kuirejesha afya yangu ndani ya muda mfupi.Nilidhani mapaja yangu hayatarejea tena katika hali yake.Mungu ni mwaminifu, kila kitu kiko vizuri kama nilivyokuwa nataka"..Ray C