Habari zinasema wawili hao walikutana Dubai hivi karibuni kabla Diamond hajaenda Malaysia na Wema akiwa njiani kuelekea Hong Kong, China ambapo walikula bata kwa sana.
Ikazidi kuelezwa kuwa wameamua kuwa kwenye uhusiano wa siri na lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha mpenzi wa sasa wa msanii huyo wa Bongo Fleva, Penniel Mungilwa ‘Penny’ hajui kitu chochote.
TAARIFA ILIVYO
Kwa muda wa siku nne, ndani ya mitandao ya kijamii hasa kwenye Instagram, maneno yenye kuashiria kuwa wawili hao wapo pamoja tena yamekuwa yakichukua nafasi.
Baada ya kusambaa kwa habari hizo, Penny naye alitupia picha yake akiwa kitandani na Diamond na kuandika kuwa waachwe kama walivyo.
Ndani ya mtandao wa Instagram yakazuka makundi mawili, upande wa mawifi wa Penny, akiwemo Halima Kimwana na kundi lingine la mawifi wa upande wa Wema.
Kundi la Wema waliandika kuwa mwanamke anayependwa na ndugu wa mume siku zote mwanamme huwa hampendi hivyo Wema ni mpenzi sahihi wa Diamond kwa vile hapendwi na ndugu kama Penny.
MBAYA ZAIDI
Mbaya zaidi, katika hali isiyotegemewa kwenye akaunti yake ya Instagram, Wema alitupia wimbo mpya wa Diamond uitwao My Number One na kuweka maoni yake kwamba anaupenda wimbo huo.
Wengine waliochangia walisema Wema ana lake jambo kwa Penny kwa vile si jambo jepesi kusifia wimbo wa mwanamme ambaye alikuwa mpenzi wake na sasa ana mwingine anayejulikana, yaani Penny.
PICHA YA WEMA SASA
Wema hakuishia kuposti wimbo huo tu, alikwenda mbele zaidi kwa kutupia picha yake yenye pozi tamu na kuuliza; huyu hapa baby wa nani huyu? (yaani yeye).
Wengi walimsifia lakini wengine walifunguka kwa kusema ni baby wa Diamond, jambo ambalo Wema hakulipinga.
PENNY AONGEA NA AMANI
Kufuatia kuenea kwa habari hizo, Amani lilianza kuwasaka watu watatu ambao ndiyo wenye uwezo wa kubainisha ukweli au uongo wa ishu hiyo iliyoenea mjini.
Watu hao ni Diamond mwenyewe, Wema anayedaiwa kurudiwa na Penny, mpenzi wa sasa wa Diamond.
Wa kwanza kupatikana alikuwa Penny ambapo alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa madai hayo alifunguka:
AKIRI KUNYETISHIWA
“Ni kweli hata mimi nimenyetishiwa habari hizo lakini siamini kama inawezekana hao watu wakarudiana.
ASEMA KUNA KUNDI LINAPANGA NJAMA
“Nijuavyo mimi kuna kundi la watu ambao wapo upande wa pili (wa Wema) ndiyo wanaoeneza hizo habari, pengine wanataka niamini kisha nimwache Diamond, simuachi ng’o.
ANATAKA USHAHIDI
WA PICHA
“Kama niliweza kumvumilia kwa kuona picha akiwa na Irene Uwoya hotelini sembuse hili la safari hii hata picha hakuna?”
ALISHAMUULIZA DIAMOND
“Mimi nilishamuuliza Diamond, japo hakusema ni kweli au uongo ila aliniambia achana na hizo habari.”
DIAMOND APIGA KIMYA
Baada ya kuongea na Penny,
lilimpigia simu Diamond ambapo alipokea na kusema yuko kikaoni na kumtaka paparazi kupiga baadaye. Hiyo ilikuwa saa 4:16 asubuhi ya juzi.
Saa 7:11 mchana, Diamond alipigiwa simu tena lakini hakupokea. Akatumiwa meseji ya kumkumbushia, hakujibu. Akatumiwa meseji yenye madai ambayo pia hakuijibu.
MAMA WEMA KABLA YA KUULIZWA AFUNGUKIA MADAWA YA KULEVYA
Amani liligundua Wema bado yupo Hong Kong hivyo liliamua kumpigia simu mama yake, Bi. Miriam Sepetu ili kuomba namba ya bintiye, lakini kabla ya ombi hali ikawa hivi:
“We nani, hivi kuna gazeti moja limeandika eti mwanangu amekamatwa na madawa ya kulevya China anasubiri kunyongwa, ni akina nani wale, wana akili kweli?
“Mimi sikubali safari hii, tutafikishana kwa mwanasheria wangu.
“Tena ukikutana nao waambie waache kumzushia mwanangu, wasimtie mkosi bure, hajakamatwa yupo salama kabisa.”
Mpaka sasa ushahidi wa kuonesha wapenzi hao wa zamani kuwa wamerudiana bado haujawekwa hadharani.
GPL