Like Us On Facebook

POLISI WATUMIA NGUVU KUWATAWANYA WANANCHI WALIOKUWA WAKIIBA MAFUTA BAADA YA LORI KUPINDUKA

                 Askari wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro wamelazimika kutumia nguvu  kuwatawanya wananchi  na kuwachapa viboko watu  waliokuwa wakiiba mafuta mara baada ya ajali la lori liliosheheni mafuta aina ya Dizel lililokua likitokea jinini Dar es Salaam kuelekea Zambia kupinduka katika eneo la Msamvu mjini Morogoro.

 ITV imeshuhudia baadhi ya wananchi wakiwa na ndoo na madumu huku kukiwa na mvutano  mkubwa  kati  yao  na  polisi ambapo wananchi hao  wametupia lawama askari wa jeshi la polisi kuwafukuza kwa madai  kuwa  hawaoni sababu kwani kuanguka kwa gari hiyo imekuwa ni fursa kwao.
 

Nae mkuu kituo cha usalama barabarani mkoa Morogoro wa Leonard Fungu akizungumzia tukio hilo amesema wamelazimika kutumia nguvu kuwatawanya wananchi waliokuwa wakiiba mafuta kwani wizi  wa mafuta kwenye matukio ya ajali si kitendo cha uungwana pia wanaweza kuhatarisha usalama wa maisha yao.


Ajali hiyo imetokea wakati  dereva wa lori alipokuwa akikata kona . Gari lilimshinda na kupinduka .
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari