Like Us On Facebook

MSANII TEJA AOLEWA


           Msanii wa maigizo nchini, Bahati Abilah ‘Kisoki’, ambaye mara nyingi anaigiza kama teja la kike  wiki iliyopita alifunga ndoa na Muhaji Salim nyumbani kwao Temeke jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali.
Akizungumza na paparazi wa Ijumaa huku akiwa mwenye furaha, Kisoki alisema kuwa anamshukuru sana mumewe huyo kumuoa kwani ni wanaume  wachache wanaoweza kuzikubali kazi za wapenzi wao hususan za kisanii na kufunganao ndoa.
Kisoki aliongeza kuwa, kwa jinsi anavyoigiza kama teja la kike na baadhi ya watu kumchukulia hivyo ingekuwa vigumu kuolewa lakini baada ya mchumba wake kujua ilikuwa kazi kama zingine wamefunga ndoa.
 “Unajua watu wengi sana wanajua mimi ni teja kweli la kike kitu ambacho si kweli, hivyo mwanaume  anayekuona kupitia michezo yako na akakupenda kutoka moyoni kama ilivyotokea kwangu ndiye mwanaume wa kweli na nitadumunaye,” alisema Kisoki.

-GPL
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari