Like Us On Facebook

HALI YA BANZA STONE INAZIDI KUWA MBAYA AOMBA MASHABIKI WAKE WAMUOMBEE!!



NGULI wa muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ ameanza kuugua tena ambapo tangu Sikukuu ya Iddi hadi sasa yupo hoi kitandani.

Akizungumza kwa huzuni na mwandishi wetu, Banza alisema alipomaliza shoo ya Sikukuu ya Iddi na Bendi ya Extra Bongo, alianza kuugua, akaenda Hospitali ya Yemen iliyopo Sinza, Dar ikagundulika ana malaria kali ambapo alipewa dozi ya siku saba.



“Nilipewa dawa za malaria nikameza nikaambiwa baada ya siku saba nitajisikia vizuri lakini mpaka sasa sioni mabadiliko yoyote, bado mwili unaniuma sana, nashinda kitandani kila siku hivyo muziki basi kwa sasa,” alisema Banza na kuongeza:
 

“Najua mashabiki wangu watanimisi lakini kwa sasa muziki nimepumzika, naomba mashabiki waniombee.”

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari