Like Us On Facebook

TAZAMA JINSI MCHEZAJI WA YANGA "CHUJI" AKIPAMBANA NA POLISI KWA KUTAKA KUMPIGA REFA KWENYE MECHI YA JANA...!!!

Askari Polisi wakimzuia Kiungo Mkabaji wa Yanga, ambaye ni majeruhi, Athuman Idd 'Chuji' aliyechukizwa na uchezeshaji mbovu wa mwamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Coastal, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, leo jioni. 

Chuji alikuwa akimsaka mwamuzi huyo ili kumtia adabu kutokana na maamuzi yake ya kuwapa penati wapinzani wao ambayo wao waliielezea kuwa haikuwa sahihi. Mwamuzi huyo Martin Saanya, alitoa penati katika dakika ya 90+ kwa kile kilichoonekana kuwa Beki wa Yanga David Luhende aliunawa mpira huo, huku mshika kibendera wake akiwa karibu kabisa na eneo la tukio na kushindwa kutoa maamuzi kwa kumsaidia mwamuzi wake ambaye alipuliza kipyenga cha kuashiria mkwaju wa penati hiyo iliyowakasilisha mashabiki na wachezaji wa Yanga.

Katika mchezo huo Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia mshambuliaji wake, Didier Kavumbagu, katika dakika ya 68, kufuatia pasi nzuri iliyopigwa na David Luhende, na Coastal, walisawazisha bao hilo kwa mkwaju huo wa penati uliopigwa na Jerry Santo. 

HUKO KWINGINEKO Matokeo ya mechi za leo ni:- Rhyno 0-Azam 2, Oljoro 0- Simba 1, Tanzania Prisons 0- JKT 3, Ruvu Shooting 1- Mbeya City 2, Mgambo Shooting 1- Ashanti Utd 0, Mtibwa Sugar 1- Kagera Sugar 0
 Kipa wa Coastal Union, Shaban Kado, akiruka kuokoa moja ya hatari langoni kwake.
 Beki wa Coastal, Juma Nyoso (wa pili kushoto) akiondosha hatari, huku wachezaji wa Yanga, Hussein Javu (kushoto) na hamis Thabit, wakiwania mpira huo.
 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (katikati) akiwatoka mabeki wa Coastal.
 Mabeki wawili wa Coastal, wakimdhibiti David Luhende.
 Didier Kavumbagu, akishangilia bao lake sambamba na Simon Msuva. Katika mchezo huo mwamuzi alitoa kadi nyekundu kwa wachezaji wawili Simon Msuva na wa Coastal.
Askari Polisi wakilinda mlango wa Chumba alichoingia Mwamuzi wa mchezo huo baada ya kuona usalama wake matatani, ambapo Chuji alijaribu kupangua ngome hiyo ili kuufikia mlango huo bila mafanikio.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari