Like Us On Facebook

NYAMA NA MAINI YA NG'OMBE YASABABISHA JAMAA KUMUUA MKEWE HUKO SINGIDA



Mkazi wa kijiji cha Minyughe, wilayani Ikungi, Bonphace Misanga (70) anashikiliwa na polisi mkoani Singida,kwa tuhuma za kumpiga mkewe Amina Kunyonga (67) hadi kufariki dunia baada ya kuzuka mabishano ya nini kianze kupikwa kati ya nyama na maini.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne wiki hii.



Alisema siku hiyo wanandoa hao walikwenda kwenye mnada kijijini hapo na baada ya kunywa kiasi kingi cha pombe ya kienyeji walikubaliana wanunue nusu kilo ya maini na nusu ingine ya nyama mchanganyiko ya ng'ombe, huku wakiwa tayari wamekwisha lewa.

Kamanda Kamwela alisema baada ya kufika nyumbani mume alimwagiza mkewe aanze kupika nyama ya maini lakini mkewe akadai anataka aanze na nyama mchanganyiko.

"Baada ya kufika nyumbani, baba mwenye nyumba alimtaka mke aanze kupika maini halafu baadaye amalizie na nyama ya ng'ombe mchanganyiko, lakini badala yake mkewe alikataa akamwambia mtuhumiwa kuwa ataanza kwanza kupika nyama ya ng'ombe kwa madai kuwa huchukua muda mrefu kuiva,"alifafanua Kamwela.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari