Mke wa Sheikh Ponda, Mariam Ponda.
Mama huyo alitia simanzi hiyo wakati mumewe alipofikishwa mahakamani hapo kwa mara ya pili kwa ajili ya muendelezo wa kesi ya uchochezi inayomkabili.
Akiwa mahakamani hapo, baada ya mumewe kusomewa mashitaka matatu yanayomkabili na wanasheria wake, Bernard Kongola na Sunday Hyera kukana, mwanamke huyo alikimbilia mlangoni ili kumsabahi kwa kushikana naye mikono lakini ilishindikana.
Sheikh Ponda akiwa kizimbani leo.
Ilimuuma sana, machozi yalimlenga machoni ambapo alilazimika kujifuta kwa baibui alilojitanda huku akiinamia chini kwa huzuni.
Hata hivyo, mwanamke huyo hakukata tamaa, mumewe alipopandishwa kwenye gari la kumrudisha Segerea Dar, alilifuata na kutaka kumpa mkono lakini alizuiwa na maafande wa magereza waliokuwa wakimlinda, kitendo kilichomfanya ainame tena kwa huzuni.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 11, mwaka huu na mtuhumiwa huyo amerudishwa gerezani
Source:GPL.