Like Us On Facebook

IRENE UWOYA AJIBU MAPIGO KWA WEMA,VITA YAIBUKA

Vita mpya imeibuka ikiwahusisha warembo wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Irene Pancras Uwoya kufuatia kuanzisha vipindi vya runinga kwa mpigo.
                                                        Irene Pancras Uwoya.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, katika harakati za vipindi hivyo, alianza Wema kwa kuanzisha ‘aidia’ ya kipindi kipya kiitwacho In My Shoes ambacho kitaanza kuoneshwa kuanzia Alhamisi hii, saa tatu na nusu usiku kupitia Clouds TV.


                                                                Wema Isaac Sepetu.
Alisema baada ya Wema kutengeneza kipindi hicho na kupata maoni mengi, Uwoya akajibu mapigo kwa kuanzisha cha kwake kinachoitwa Paradise ambacho kitakwenda hewani Jumanne hii (kesho).
“Mashabiki wa Clouds TV watapata kuona vita ya kibiashara, Uwoya atakuwa akionekana katika kipindi hicho ambacho kitakuwa kinahusu upakaji rangi katika nyumba za watu mbalimbali huku Wema naye akikimbiza katika In My Shoes,” alisema Ruge.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari