Akiongea na mwandishi wetu hivi karibuni, Matumaini alisema kwa sasa anaendelea vizuri na ameshaanza kucheza filamu mbalimbali anazoshirikishwa na wasanii wenzake na sasa anaendesha maisha yake mwenyewe.
“Nawashukuru sana wasanii wenzangu kwani kama siyo wao, ningerudishwa nikiwa maiti, sina cha kuwalipa ila Mungu ndiye atakayewalipa,” alisema Matumaini.
Hata hivyo, alilaani vikali baadhi ya wasanii wanaozusha maneno ya uongo kwamba Michael Sangu alikula fedha alizokuwa anachangisha kwa ajili yake jambo ambalo siyo la kweli.