Ray C anayetarajia kurejea kwenye ‘game’ hivi karibuni, akasema anaamini yeye ni msichana imara kutokana na namna alivyokuwa akipambana na sasa ni Ray C mpya.
Aliandika hivi: “The New Ray C, am strong lady (Ray C mpya, mimi ni msichana imara)…kila nipewapo mtihani mgumu wa maisha napigana mpaka nakuwa mshindi.”
Pia kupitia mtandao huo, Ray C alitupia video ambayo anasikika akiimba wimbo wa msanii wa THT,Winfrida Josephat ’Recho’ uitwao Upepo kisha akaandika: “I love your voice my sis.” Recho akajibu: Thanks a lot my dada.”