
Akiongea  na  mwandishi wetu  juzikati jijini Dar es Salaam, Madaha 
alisema ishu ile imemsababishia matatizo makubwa ya kifamilia na hata 
kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima ulivyokuwa.
Alisema filamu anayoisambaza kwa sasa na kibao chake cha mwisho 
kukitoa cha Mr. Dj ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya sanaa kwa 
upande wake.
“Nimeamua
 kuachana na sanaa kabisa, siwezi kuishi maisha ya presha yasiyo na 
uhuru. Nitarudi kwenye fani yangu niliyosomea (hakutaka kutaja), maana 
naishi maisha ambayo hayana amani kabisa,” alisema.

