MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga maarufu kama 
Linah, anadaiwa kupewa ujauzito na kijana mmoja wa Kihindi anayejulikana
 kwa jina moja la Nagar.
Chanzo cha uhakika kimeliambia gazeti hili kuwa msichana huyo 
aliyeibukia kutoka kituo cha kukuza vipaji cha THT, amekuwa karibu na 
Mhindi huyo anayedaiwa kuishi Mbezi jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu 
sasa na kwamba mimba hiyo imeonekana kumfurahisha sana msanii huyo.
“Huyu Nagar ni mpenzi wake wa muda mrefu na inaonekana hii mimba 
ameipenda sana. Kila siku anamsifu huyo mpenzi wake,” kilisema chanzo 
hicho kilichodai kuwa wawili hao wamekuwa wakiambatana pamoja katika 
sehemu mbalimbali za starehe.
Chanzo
 hicho kilisema Linah alikutana na mdosi huyo katika harakati zake za 
kimuziki na kwamba jamaa ameoza mno kwa binti huyo, mkali wa albamu ya 
Atatamani.
Linah alipopigiwa simu mara ya kwanza hakupokea, lakini baada ya 
kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa kuhusu suala hilo, alipiga 
simu na kukanusha vikali tuhuma hizo.
“Nani
 kakwambia kama nina mimba? Hakuna kitu kama hicho, hayo ni maneno ya 
watu wanasambaza mtaani, mimi hata sijui wananitaka nini,” alisema.
Alipoulizwa kama hata yeye amewahi kusikia habari hizo, alisema 
anazisikia na kusisitiza kuwa siyo za kweli. Lakini alipotakiwa kusema 
kama anamfahamu Nagar, alimtaka mwandishi kuachana na habari hizo.
“Wewe
 si umeuliza habari za mimba? Sasa hayo mengine yanatoka wapi, 
ulichotaka kujua nimekujibu, hayo mambo mengine achana nayo,” alisema 
bila kufafanua zaidi

