Like Us On Facebook

MGANGA WA DIAMOND ATABIRI DIAMOND KUFULIA KIMUZIKI NA KIFEDHA HIVI KARIBUNI

Mtu mmoja anayedai kuwa mganga aliyemtoa mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameibuka tena na kueleza kuwa Diamond Platinumz tayari ameanza kushuka kimuziki kama alivyosema awali.
Mtu huyo anayejitambulisha kwa jina la Dr. Yahya Michael ameuambia mtandao wa mamuafrica kuwa kile alichokisema mwanzo kuwa Diamond Platinumz atashuka kimuziki na kurudi pale alipokuwa kimeanza kutokea ingawa watu wengi hawaoni.
“Diamond alikuwa anapiga show kwa milioni 10 lakini sasa hivi hapewi hata show ya milioni 7. Nilizungumza kushuka sio kupanda na nashukuru kwa sababu rekodi ninayo. Nimeongea kushuka sio kupanda, wale walioko nyuma yake hivi sasa ndio wanaonekana kuongoza. Hata katika mambo yenu ya kumi bora za Tanzania yeye hayumo katika mbili.” Amesema Dr. Yahaya

“Sijawahi kumuona mtu anaepanda anaambiwa ameiba nyimbo, sijawahi kuona mtu anaepanda anashindwa na yule ambaye alikuwa anamshinda mwaka jana. Na wala sijawahi kumuona mtu anaeambiwa anapanda halafu anapigwa mawe na watu waliokuwa wanataka wamuone kwa kiingilio kikubwa.” Ameeleza.

“ Kwa sababu Diamond wa mwaka 2010,2011,2012 ni Diamond aliyekuwa anapiga show Mlimani City sehemu alipozaliwa Dar es Salaam kwa kiingilio cha shilingi 50,000, siku tatu kabla ya tukio tiketi zimekwisha. Kwa hiyo Diamond wa hivi sasa ni yule ambaye anapiga show Tabora sehemu ambayo hajawahi kuonekana, kwa kiingilio cha shilingi 5,000 na watu hawaingii na bado walioingia wanampiga mayai viza na mawe.” Ametoa mchanganuo wake.
Mtu huyo akafika mbali na kuapa, “ amini, sitakufa kabla haki hii haijatendeka, naapa…kwa heshima ya mwenyezi Mungu aliyeniumba. Anasema pigania chako ali hali hata ukifa ili mradi ulikuwa unapigania chako.”
Hata hivyo, Naseeb Abdul aka Diamond aliwahi kumkana Dr. Yahya na kueleza kuwa hamfahamu na hajawahi kumuona.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari