Ray na Chuchu wakijiachia.
Chanzo chetu makini kilieleza kuwa mastaa hao wamekuwa wakionekana
pamoja mara nyingi na hivi sasa inadaiwa kuwa wanaishi pamoja huku
wakiwa na mtoto wa Chuchu aitwaye Danzel.
Mpashaji wetu huyo alizidi kudai kuwa kutokana na mapenzi hayo
kukolea siku hadi siku, juzikati baadhi ya ndugu wa mastaa hao walianza
vikao vya chini kwa chini ili kuhakikisha mwaka huu wasanii hao
wanafunga ndoa lakini haijajulikana kama watafungia kanisani au
msikitini kwa kuwa wana dini tofauti.
“Yaani sasa hivi hakuna siri hata chembe, ni fulu kujiachia. Mara
nyingi wapo pamoja kila sehemu yaani kama njiwa,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo
hicho kilizidi kudai kwamba mara nyingi Ray na Chuchu wanapenda kwenda
kuogelea na kujiachia kama mke na mume kwenye hoteli moja maarufu (jina
linahifadhiwa) iliyoko maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar huku wakijifotoa
picha za kumbukumbu.
Baada ya kujazwa ‘info’ hizo na kumwagiwa picha za mastaa hao, gazeti
hili lilimtafuta Chuchu kisha kumuuliza kuhusiana na penzi lake na Ray
kuwa ‘shatashata’ ambapo alifunguka kuwa kama kuna mtu anawaona wakiwa
pamoja ni kwa sababu hivi sasa eti wanaandaa ‘sinema’ yao wawili.
Alipotafutwa Ray ili kuulizwa kuhusiana na ishu hiyo, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa kwa muda wa nusu saa