Wakati tunaelekea katika ile siku inayoaminika kuwa siku ya wapendanao ‘Valentine’s Day’, mkali wa Valuvalu Jose Mayanja Chameleone ameamua kumuonesha mkewe Daniella na dunia nzima jinsi anavyompenda, kwa kujichora tattoo yenye jina lake shingoni.
Chameleone ambaye yuko nchini Afrika Kusini kwa shughuli za kimuziki,
alipost picha hizo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, picha
zinazoonesha tattoo hiyo hata mtu akimuona kwa mbali kidogo.
Mwimbaji huyo wa Valuvalu ambaye ana watoto watano aliozaa na mkewe
Daniella hakuwasahau wanae pia, alijichora katika mkono wa kushoto
tattoo yenye majina manne ya wanae wanne na anatarajia kuongeza moja
yenye jina la mwanae wa kwanza, Ayla.
“2014 we stand tall for the ones we care for and those that love us
back with their whole. For me, this is my expression..” Amesema
Chameleone.