Like Us On Facebook

TAZAMA TASWIRA YA KIJIJI CHA QUNU ALIKOZIKWA MZEE NELSON MANDELA JUMAPILI DESEMBA 15, 201‏3

 Daraja la waendao kwa miguu likipita juu ya barabara mpya ya lami inayojengwa kuelekea kijijini Qunu.
Siku ya mazishi barabara ya kuelekea Qunu ilifungwa na ni magari yaliyokuwa na kibali tu ndiyo yaliyoruhusiwa kupita
Ulinzi ulikuwa mkali kila sehemu kijijini Qunu.
Wageni wakiwa katika geti kuu la nyumba ya Mzee Mandela hapo Qunu.
Nyumba ya Mzee Mandela.
Nyumbani kwa Madiba kijijini Qunu.
Hema maalumu zilikofanyika shuguli zote za mazishi. Kaburi lake liko nje ya hema upande wa kushoto.
Hali ilivyokuwa saa kumi na moja alfajiri siku ya Jumapili.
Nyumbani kwa Madiba kumejaa magari hata kabla ya jua kupanda angani.
Sehemu ya kijiji cha Qunu. Mahema mbele ya nyumba ni ya wanahabari wa kimataifa waliopiga kambi hapo.
Mandhari ya Qunu.
Mandhari ya Qunu.
Ni kijiji chenye mandhari nzuri. Wakati wa majira ya baridi barafu huanguka hapa.
Qunu.
Kila engo Qunu inapendeza.
Kijiji cha Qunu.
Bango linalotangaza kijiji cha Qunu kuwa cha urithi.
Ulinzi ulikuwa si wa kawaida siku ya mazishi.
Foleni ilikuwa ya kufa mtu.
Wana Afrika Kusini toka kila kona walitembea umbali mrefu kwa miguu kuhudhuria mazishi.
Nyimbo na ngoma vilitawala.
Mdau aklipoza koo baada ya kutembea kwa muda mrefu.
Sehemu ya mji wa Mthatha, kilomita kama 32 kutoka Qunu.
Magari yalizuiwa kwa muda wakati mwili wa Mzee Madiba uliopowasili uwanja wa Mthatha na kupelekwa Qunu.
Sehemu ya foleni ya magari ikikaribia mji wa Mthatha na hapa wakisubiri msafara wa mwili wa Mzee Mandela upite
Qunu ni kijiji kidogo katika jimbo la Eastern Cape la Afrika Kusini, kilomita 32 Kusini-Magharibi ya mji wa Mthatha, katika barabara ya Butterworth na Mthata. 

Kijiji cha Mvezo, pembezoni mwa mto Mbashe, ni jirani ya mahali ambapo Mzee Nelson Mandela alizaliwa. Hapo Qunu ndipo alipokulia na aliweka nadhiri ya kurejea. Kijiji cha Qunu ndipo baba yake Mandela alipohamia baada ya kuvuliwa Uchifu wa Mvezo. Katika kitabu chake cha ‘Long Walk to Freedom’ Mzee Mandela amekitaja kijiji hicho kuwa ndipo alipoishi maisha ya furaha wakati wa utotoni.Jumapili ya Desemba 15, 2013 Mzee Mandela alizikwa kijijini Qunu katika mazishi ya Kitaifa yaliyoshuhudiwa dunia nzima. Alizikwa kwa heshima zote za kiongozi wa Taifa katika sehemu aliyochagua mwenyewe kuwa nyumba yake ya milele.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari