Madaktari wakiwa wameunganisha mkono wa Xiao kwenye kifundo cha mguu wakisubiri apone majeraha mengine ili waurudishe eneo lake.
Madaktari wakiuangalia mkono wa Xiao Wei kabla ya kumfanyia oparesheni kuurudisha eneo lake.
Xiao Wei baada ya kurudishiwa mkono wake. (Picha Zote na Rex)"Nilishtuka sana na kushindwa kuondoka eneo hilo mpaka wafanyakazi wenzangu walipoondoa mashine na kutoa mkono wangu kisha kunipeleka hospitali" Alisema Xiao, akielezea ajali hiyo iliyotokea mwezi uliopita.
Baada ya kupelekwa katika hospitali mahiri nchini China, saa saba baada ya ajali hiyo, madaktari walisema wataurudisha mkono huo ila siyo moja kwa moja.
Ili kuzuia mkono wa Xiao usiharibike, madaktari waliamua kuuunganisha katika kifundo cha mguu ambapo ulikaa kwa mwezi mzima baada ya kupona majeraha mengine ndipo walipourudisha katika eneo lake. Madaktari wanadai Xiao atapona vizuri na mkono wake utafanya kazi kama zamani.
-Metro

