Akiutangazia Umma wa wakazi wa Afrika ya kusini hapo jana Rais wa Nchi hiyo bwana Jacob Zuma alisema maneno yafuatayo: "Our nation has lost its greatest son, yet what made Nelson Mandela great was precisely what made him human," "We saw in him what we seek in ourselves, and in him we saw so much of ourselves."

Bwana Nelson Mandela aliyekuwa akisumbuliwa mara na maradhi mbali mbali Ikiwemo figo na viungo vingine vya mwili kufikia hali ya kushindwa kufanya kazi hali iliyomlazimu Mkongwe huyo wa siasa Barani Afrika kupuma kwa kutumia mashine maalum,
Nelson Mandela atakumbukwa kwa Juhudi zake katika kuleta Ukombozi Barani Afrika na bado anabaki kama Alama ya Ushindi kwa Bara hilo huku Akiwaachia Simanzi kubwa Wakazi wa Nchi Hiyo ambao Mpaka sasa wanaonesha kutoamiani kilichotokea.
HISTORIA FUPI YA MANDELA.
Nelson
 Rolihlahla Mandela ni Rais wa kwanza Mwafrika wa Afrika Kusini ya 
kidemokrasia. Ni mtu aliyejijengea heshima kubwa duniani kutokana na 
jitihada zake kubwa zilizofanikisha uhuru wa nchi hiyo na nyinginezo 
katika Bara la Afrika.
Mzee Mandela anayefahamika pia kwa jina la Mzee Madiba amelazwa 
hospitalini mjini Pretoria, Afrika Kusini kwa zaidi ya mwezi sasa akiwa 
mahututi. Anasumbuliwa na ugonjwa wa mapafu.

Kutokana na umaarufu wa Rais huyo mstaafu wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 95, JAMHURI tumeona vema kuchapisha historia fupi ya maisha yake kama ifuatavyo:
Nelson
 Mandela ni mwanasiasa mkongwe na mwanaharakati aliyepambana na sera za 
ubaguzi za makaburu wa Afrika Kusini na hatimaye kuwa Rais wa kwanza 
Mwafrika nchini humo. Ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel. Pia amepata 
kutunukiwa zaidi ya tuzo 250 katika miongo minne iliyopita.
Ni
 rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. 
Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa Chama cha African National Congress
 (ANC) aliyepinga utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.
Nelson
 Mandela alizaliwa Julai 18, 1918. Baba yake mzazi alifariki wakati 
Mandela akiwa na umri wa miaka tisa. Tangu kipindi hicho alilelewa na 
Jonintaba hadi alipoitoroka familia hiyo baada ya kutakiwa aoe mwanamke 
aliyepangiwa.
Mwaka 1943 Mandela alijiunga ANC. Aliiongoza Afrika ya Kusini dhidi ya ubaguzi wa rangi na kuibuka kiongozi shujaa duniani.
Alipoanza
 mapambano ya kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi na kutafuta usawa kwa 
wote, ilitegemewa kuwa mke wake ndiye angekuwa mstari wa mbele katika 
kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
Mandela
 alipata kuoa wake watatu katika historia ya maisha yake. Alimuoa mke wa
 mwisho siku alipokuwa akiadhimisha miaka 80 ya kuzaliwa kwake.
Madiba
 anatajwa kuwa katika kipindi chote cha historia yake amekuwa akiwaunga 
mkono watoto na upatikanaji wa elimu. Mfuko wa Nelson Mandela wa 
kusaidia watoto ni sehemu tu ya ushahidi wa mafanikio ya Mandela 
kuwasaidia watoto.
Mandela
 ni baba wa watoto sita. Watoto wanne aliwazaa na mke wake wa kwanza, 
Evelyn Mase na watoto wawili aliwazaa na mke wake wa pili, Winnie 
Madikizela.
Inaelezwa kuwa baadhi ya watoto wake hawakupata kwenda kumwona Madela alipokuwa gerezani.
Watoto wake wote wawili wa kike aliowazaa na mke wa kwanza walikuwa wakitumia jina la Makazawie.
Mtoto
 wake wa kwanza alifariki akiwa na umri wa miezi tisa na mtoto wa pili 
aliyejulikana kwa jina la Madiba Thembikile (Thembi) alifariki katika 
ajali ya gari mwaka 1969 akiwa na umri wa miaka 25. Mandela alikuwa 
gerezani na hakuruhusiwa kwenda kuhudhuria mazishi ya mwanaye.

Mtoto
 mwingine, Makgatho alifariki kwa ugonjwa wa Ukimwi mwaka 2005. Mandela 
amekuwa mstari wa mbele kupiga vita virus vya Ukimwi na Ukimwi akitumia 
namba 46664 ambayo ni namba yake alipokuwa gerezani kupiga kampeni.
Mandela
 na Evelyn walidumu katika ndoa yao kwa miaka 13 kabla haijavunjika 
mwaka 1957. Evelyn alikuwa muumini wa dhehebu la Mashahidi wa Yehova 
lililokuwa haliruhusu waumini wake kushiriki kwenye siasa, hivyo muda 
wote hakujihusisha na siasa. Alifariki mwaka 2004.
Mandela
 alimuoa Winnie Madikizela mwaka 1958, ingawa muda mwingi hawakuishi 
pamoja kwa sababu alikuwa kifungoni huku Winnie akijijengea umaarufu 
katika majukwaa ya siasa.
Kutokana
 na misuguano iliyoibuka ndani ya umaarufu wa kisiasa ya Mandela na 
Winnie walijikuta wakipeana talaka mwaka 1994. Mwaka 1998 Mandela 
alimuoa Graca Machel ambaye alikuwa mke wa kwanza wa Rais wa Msumbiji, 
Samora Machel.
Rais
 wa sasa wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ameendelea kutoa wito kwa 
wananchi wa nchi hiyo wamwombee heri wakati huu anapougua. Maombi 
yamekuwa yakifanywa makanisani kote nchini Afrika Kusini kumwombea 
Mandela apone maradhi yanayomsumbua.
Hata
 hivyo, Mandela ameshaandika wosia wake na kuelekeza kwamba kama atakufa
 azikwe kwenye milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu zake huko Qunu, 
Afrika Kusini.
Mandela
 alikuwa Rais wa Afrika Kusini kuanzia mwaka 1994 hadi 1999. Alifungwa 
jela miaka 27 kuanzia mwaka 1962 hadi mwaka 1990. Anaelezwa kuwa 
alikumbwa na ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika 
machimbo ya mawe akiwa gerezani.
Gumzo
 la jiji Tunaungana na Wananchi wa Afrika ya Kusini Wengine wote duniani
 wenye Mapenzi mema kwa kuomboleza Msiba huu Mzito wa kuondokewa na 
Kipenzi chetu mzee NELSON MANDELA
Mungu Ailaze mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Amina  

