Hivi
ndivyo alivyosema Rage ‘Mimi najiuliza ndo maana nimeomba ufafanuzi
toka Fifa baada ya kufika tu,mi nilikua sipo nchini kwa mwezi mzima
nimeandika barua kwenda Fifa jana ile ile na pia Tff tumeandika barua
kwa niaba ya Simba ili kutoa malalamiko yetu,kwa sababu hata sisi
inatuchanganya huyu mchezaji mkataba wake,labda kama kuna ushahidi
watuonyeshe kama Fifa wamevunja mkataba na Etoile du Sahel lakini
ukisoma kwenye mtandao wa Fifa kuna kesi 3 ziko pending’.
‘kesi
ya Simba kuidai Etoile du Sahel kuna kesi ya Etoile du Sahel
kulalamika mchezaji wao ametoroka,kuna kesi ya Emanuel Okwi kudai pesa
zake hajalipwa na Etoile du Sahel,kwa hiyo huu ujanja uliotumika sijui
umetokea wapi tumelalamika Fifa wakati tunamtoa Villa walisema
wamempeleka Villa kwa mtaba wa miezi 6 na miezi 6 haijaisha,jana nimeona
kwenye luninga moja wanaonyesha ITC ile ITC kila club Tanzania
inawezaa kuprint tu.’
‘Uganda
matatizo yao walisaidiwa kutatuliwa kwa haraka na chama chao cha mpira
cha Uganda sisi chama chetu hapa lazima niseme ukweli hawajatusaidia vya
kutosha wamelala kwa muda mrefu sijui kwa sasa hivi kwa sababu
amekuja mheshimiwa Malinzi labda wataanza kusaidia vilabu vytu
kuhakikisha tunapata haki zetu kwa sababu Fifa wana utaratibu wao wa
kuheshimu wanachama wao wanatoa uzito kwa mfano Sector General wa Fifa
anaweza kuongea na Sector General wa tff lakini si mimi President wa
Simba,siwez kuongea na Sector General wa Fifa moja kwa moja mi naongea
na makanjanja tu’.
‘Kwenye
sheria tuna kitu kinaitwa Legal Status Kwa wanachama wa tawi la Mpira
Pesa hawana hadhi ya kisheria ya kuongea masuala ya simba maana hao si
tawi la simba lililosajiliwa hawana hata hiyo hati na haiwezekani katika
matawi 78 tawi 1 tu kila siku wanaongea mi wangeongea matawi 78 kidogo
ningeshtuka ,mimi nimechaguliwa na watu 1,820 sasa tawi la mpira pesa
sijui lina watu 204 sijui 100 ila hata sielewi lina watu
wangapi,haliwezi kunipa taabu’.
‘Sina
nia ya kuitisha mkutano wa dharura kama hali itaendelea hivi ya
kutoelewana njia nyepesi nayoona ndugu yangu ni kuitisha mkutano wa
uchaguzi mwezi January kabla ya tarehhe 27 Januaryili upatikane uongozi
mpya kuanzia Mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji’
‘Napitia
vifungu vya sheria nisome na ngojea uamuzi wa Tff watasema nn kuhusu
malalamiko yangu,maana baada ya maazimio ya kamati utendaji niliandika
barua kuomba kamati ya utendaji ipitie maamuzi yake ya mwanzo kulikua na
dosari nilizona na nikaeleza dosari nilizoziona kwa hiyo wakirekebisha
hizo dosari nipo tayari kufata’
‘Mimi
binafsi siwezi kufanya kazi na kamati ambayo tayari ilishanituhumu na
kunisimamisha kwa hiyo tayari hawana imani na mimi sasa mimi imani na
wao natoa wapi,kwa hiyo tutakua hatuwatendei haki wanachama wa
Simba,sasa ili tuonekane wote tunafata maadili basi ni vyema kuanzia
Mwenyekiti na Wajumbe wote wa kamati ya utendaji tukajiuzulu tukaitisha
mkutano wa uchaguzi ili kuikoa klabu yetu ili ipate mafanikio makubwa’.