MWALIMU
Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo
za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku
akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za
kishirikina.Tukio
hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, Juma
Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye kibao hicho wakati alipokuwa
anamsindikiza nduguye, Aisha Mbilimoto aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar
es Salaam.Akizungumzia
tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala
chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi) huku
akikoroma kutokana na kuwa na usingizi mzito.Alisema
awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa
alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la
kumwamsha ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda
nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwaKwa
upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa, wamekosa molari wa
kufanya kazi kutokana na kitendo alichofanyiwa mwalimu mwenzao.Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Francis Milanzi
alisema walimu shuleni hapo wamekosa amani na kuwasababishia kuzihama
nyumba zao kwa muda na badala yake kwenda kukesha kwenye ofisi za
walimu tangu tukio hilo litokee.Ofisa elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi
alisema amepokea taarifa za tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu
kuwa na subira wakati utaratibu wanalishughulikia suala hilo.Magigi
aliongeza kuwa ofisi yake itafanya utaratibu wa kumhamisha mwalimu
huyo na kumtafutia shule nyingine huku akiwataka wakazi wa eneo hilo
kujenga ushirikiano na watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao.Hili
ni tukio la pili kutokea katika halmashauri hiyo mwaka huu ambapo la
kwanza lilitokea April katika Shule ya Sekondari Ruhokwe, mwalimu wa
shule hiyo alilazwa kwenye kibao cha shule akiwa uchi wa mnyama.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.