Like Us On Facebook

MSANII WA KUNDI LA VITUKO SHOW BAADA KUCHEZEA KICHAPO CHA MBWA MWIZI SIKU ZA KARIBUNI SASA ASWEKWA RUMANDE MKOANI TANGA KWA KUMTUKANA MPENZI WAKE WA ZAMANI NA KUDAI KAMUAMBUKIZA UKIMWI


"Kazi kijeba" picha hii ni ya siku chache zilizopita baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa huyo mpezi wake wa zamani walioachana.


MSANII huyu amekuwa mgumu wa kuelewa kila akielezwa na uongozi wa kampuni ya Al-riyamy Production na wasanii wenzake kwa ujumla kuwa apunguze unywaji wa pombe kupita kiasi hadi kubebwa na wananchi wenye huruma kuletwa kambini yeye huitikia na
kukiri kwamba hatorudia lakini hazipiti siku mbili lazima usikie kalewa kaenda kumtukana mpenzi wake walioachana..!

 Hivi majuzi aliripotiwa kambini na muendesha baiskeli (bodaboda) kwamba alimkodi akamwambia ampeleke Usagara maeneo akanywe bia mara bodaboda anashangaa anaelekezwa mitaa isio na dalili yeyote ya kuuzwa bia..! 

Ghafla wakafika kwenye nyumba flani wakamkuta dada na mpenzi wake wametulia nje kwao wanapunga upepo, Ndipo Msanii aliposhuka kwenye baiskeli nakuanza kumporomoshea matusi ya nguoni yule dada na mpenzi wake huku akijitapa kwamba yeye ana ukimwi na kashamuambukiza huyo mwanamke kwahiyo huyo mpenzi wake mpya ajiandae kufa kwa gonjwa hatari la ukimwi...!,

Dada huyo ambaye alikuwa mpenzi wake kweli enzi hizo lakini kwasasa walishatengana aliamua kupiga simu kwa mmoja kati ya wasanii waVITUKO SHOW na kutoa malalamiko yake usiku huohuo Akakiri kutokurudia sualahilo Wasanii wenzake baada ya kufikishiwa taarifa hiyo na muendesha baikeli pamoja na simu iliyopigwa na dada huyo wamkalisha chini tena Kazi chini kama kawaida na kumuonya, Akakiri kutokurudia suala hilo. Amakweli siko la kufa halisikii dawa..! 

Cha ajabu jana kalewa tena na kuenda kumtukana dada huyo tena, Dada akaenda kuripoti polisi leo wamemtia mbaroni Kazi A.k.a Kijeba yupo kituoni


TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari