Kwa watu wengi, Huddah Monroe anaonekana kama msichana
anayefikiria kula bata tu huku masuala ya msingi katika maisha akiyaweka
pembeni. Mwakilishi huyo wa Kenya kwenye Big Brother Afrika mwaka huu,
leo amethibitisha kuwa pamoja na kuonekana mara nyingi akifanya starehe,
bado anaikumbuka famiilia yake na moja ya mafanikio aliyoyafanya mwaka
huu ni kuijengea nyumba familia yake.
“One of my biggest achievements this year.I am a proud
daughter....I'm all teary. Family first,” ameandika Huddah kwenye picha
aliyopost Instagram ya nyumba aliyoijenga kwaajili ya familia yake.
“Family first! How u grew up doesnt matter ,what u do with the rest
od ur life matters and its funny how People still stuck in my past when
the world moved on,” ameandika kwenye picha nyingine.
Hongera Huddah.