MABAO
mawili ya kiungo Jack Wilshere leo yameipa ushindi wa 2-0 Arsenal dhidi
ya Marseille ya Ufaransa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku
huu Uwanja wa Emirates.
Ilimchukua
sekunde 29 tangu kuanza kwa mchezo huo kiungo huyowa England kufunga
bao la kwanza akimtungua kipa hodari, Steve Mandanda na akfunga tena bao
la pili dakika ya 65.
Kikosi
cha Arsenal: Szczesny, Sagna, Monreal, Flamini, Mertesacker, Koscielny,
Wilshere/Walcott dk75, Ramsey, Giroud, Ozil/Arteta dk82 na
Rosicky/Cazorla dk75.
Marseille:
Mandanda, Abdallah, Morel, Romao, N'Koulou, Lucas Mendes,
J.Ayew/Valbuena dk57, Lemina/Cheyrou dk82, Gignac, Imbula/Thauvin dk57
na Khalifa.
Wilshere akimtungua kipa wa Marseille, Steve Mandanda
Shabiki mkubwa: Thierry Henry alikuwa jukwani na hapa anashangilia baada ya Wilshere kufunga
Mchezo umekwisha: Wilshere akifunga bao lake la pili usiku huu
Wilshere akishangilia baada ya kufunga bao la pili
Katika
mchezo mwingine, Chelsea imefungwa bao 1-0 na FC Basle, bao pekee la
Mohamed Salah. Mabao ya Kaka dakika ya 12, Zapata dakika ya 49 na
Balotelli dakika ya 59 yameipa AC Milan ushindi wa 3-0 dhidi ya Celtic
nchini Scotland katika mchezo mwingine wa michuano hiyo.
Mohamed Salah ameifungia bao pekee Basle ikiilaza Cheslea
Vichwa chini: Branislav Ivanovic, John Terry na John Obi Mikel wakisikitika baada ya kipigo
ns.
Amefunga: Mario Balotelli akishangilia baada ya kuifungia AC Milan