Like Us On Facebook

AIBU:MFANYABIASHARA MAARUFU DAR AFUMWA AKILA URODA NA DENTI WA SHULE YA MSINGI

MZEE mmoja kigogo wa biashara ya kuuza mbao jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alinaswa kitandani ndani ya chumba akiwa na mrembo aliyedaiwa ni mwanafunzi wa shule moja ya msingi Tegeta Wazo, Dar.Mfanyabiashara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Kyando, anasemekana amekuwa na ukaribu na denti huyo anayeitwa Fatty kwa siku nyingi, kitu ambacho kiliwapa maswali baadhi ya majirani wa nyumbani kwa msichana huyo.

Katika harakati za kuchunguza ukaribu wa msichana huyo na mtu mzima huyo, mama mdogo wa binti aligundua kuwa wawili hao wana ukaribu usiofaa.

Ikaelezwa kuwa, mama mdogo wa mwanafunzi huyo aliponyetishiwa ishu hiyo, aliandaa mtego unaofyatuka kwa kasi kuliko ule wa panya ili kumtia mikononi mzee huyo mpenda kukaa na watoto wa wenzake.

“Mtego mkali uliandaliwa, siku ya siku, ma mdogo huyo alijifanya anakwenda mbali na nyumbani, binti akaona dakika tisini za mchezo lazima aibuke kidedea wa mahaba, alimwita mwanaume huyo na kumkaribisha chumbani, kumbe arobaini zao zilikuwa zimetimia,” kilisema chanzo.
Mashuhuda wa sakata hilo walidai kuwa mama mdogo na watu wengine waliwanasa wawili hao wakiwa juu ya kitanda kama walivyozaliwa, bila kufafanua walichokuwa wakikifanya.


Ili kushika ushahidi mkononi, mama mdogo wa binti huyo na wapambe wake walipiga picha za mnato na za video kisha wakaanza kumuuliza maswali ‘mlalamikiwa’ ambaye inaaminika ni mume wa mtu.

Haikuelezwa wazi ni maswali ya aina gani aliyokuwa akiulizwa lakini inadaiwa yalihusu historia ya kujuana kwao.

 Aidha, inadaiwa kuwa mama mdogo huyo alitaka kumtwanga ndoa ya mkeka mfanyabiashara huyo lakini chondechonde zake nyingi zilimwokoa na kuahidi kurejea siku inayofuata kwa ajili ya kukata mshiko wa fidia baada ya kuambiwa binti huyo bado anasoma na shuleni kulilipwa fedha nyingi.

Habari nyingine zinadai kuwa wawili hao walifahamiana miezi kadhaa nyuma kupitia lifti ya gari ambayo mshitakiwa alimpa mrembo huyo maeneo ya Boko, jijini Dar.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari