RAIS
wa FIFA, Sepp Blatter alizomewa ile mbaya jana Uwanja wa Santiago
Bernabeu wakati Cristiano Ronaldo anafunga mabao matatu peke yake katika
ushindi wa 5-1 dhidi ya Real Sociadad kwenye Ligi Kuu ya Hispania, La
Liga.
Mashabiki wa Real Madrid walikuwa wakimzomea Blatter aliyemkandia Ronaldo hivi karibuni na kumfagilia Lionel Messi wa Barcelona.
Na
wakawa wanamuimba Ronaldo Ballon d' Or, maana yake anastahli kushinda
tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia. Ronaldo alifunga dakika ya 12, 26 kwa
penalti na 76, wakati mabao mengine ya Real yalifungwa na Benzema dakika
ya 18 na Khedira dakika ya 36. Bao la kufutia chozi la wapinzani wao
lilifungwa na Griezmann dakika ya 61.
Ronaldo
sasa amefunga mabao tisa katika mechi nne zilizopita na anaongoza kwa
mabao La Liga. Amefunga mabao 62 mwaka huu na sasa amefikisha hat-tricks
19 katika Ligi ya Hispania.
Kikosi
cha Real Madrid kilikuwa: López, Carvajal, Arbeloa, Alonso/Illarramendi
dk70, Varane, Pepe, Khedira/Isco dk77, Modric, Benzema/Morata dk83,
Bale na Ronaldo.
Real
Sociedad: Bravo, Martínez/Ansotegi dk59, José Ángel, Elustondo/Zurutuza
dk45, González, Iñigo Martínez, Vela, Bergara, Seferovic/De la Bella
dk45, Xabi Prieto na Griezmann.
Kiwango tofauti: Cristiano Ronaldo amefunga hat-trick ya 19 La Liga jana akiiongoza Real Madrid kuirarua 5-1 Real Sociedad
Celebration: Gareth Bale congratulates the No 7, though he perhaps should have got on the scoresheet himself
PANDE ZA MUNICH
KLABU
ya Bayern Munich imepaa kileleni mwa Bundesliga kwa pointi nne zaidi na
sasa imeweka rekodi mpya ya kucheza mechi 37 bila kufungwa, kufuatia
ushindi wa 3-0 dhidi ya Augsburg jana.
Jerome Boateng, Franck Ribery na Thomas Muller ndio walifunga mabao hayo.
Ushindi
huo unaifanya Bayern - ambayo mara ya mwisho ilifungwa katika ligi
Oktoba 2012 - iipiku rekodi ya Hamburg kucheza mechi 36 bila kufungwa
kati ya Januari 1982 na Januari 1983.
Unstoppable: Bayern Munich players celebrate after securing victory
Borussia Dortmund ilifungwa 2-1 na Wolfsburg. Dortmund
walitangulia kupata bao dakika za majeruhi kipindi cha kwanza kupitia
kwa Marco Reus, lakini Ricardo Rodriguez akasawazisha dakika ya 56 na
Ivica Olic akafunga la ushindi dakika ya 69.
Rare goal from defence: Jerome Boateng got Bayern off to the perfect start
Surprise: Wolfsburg's Ivan Olicscored as his side beat Borussia Dortmund 2-1