WANASEMA za mwizi arobaini, ikiongezeka moja mshukuru Mungu! Novemba 16, mwaka huu ilikuwa siku ya aibu kwa bosi Hussein Shaban (35) kufuatia kudaiwa kufumaniwa katika nyumba ya kiongozi mmoja wa Chama cha Mapinduzi (CCM) huko Tegeta jijini Dar es Salaam.
Sakata hilo la aina yake lilitokea katika kitongoji cha Nyeishozi,
Tegeta kwa kumuhusisha Hussein ambaye ni mfanyabiashara na mke wa
kigogo huyo ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa.
Akisimulia tukio zima mwanzo
hadi mwisho, kiongozi huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe , alisema miezi miwili iliyopita alianza kuhisi ndani ya ndoa
yake kuna jambo lanaloendelea kwa siri baada ya nyumba yake kupoteza
amani, mke alibadilika tabia ghafla.
“Siku moja nilikuwa natafuta nyaraka za kazini ambazo nilikuwa
nimeziweka kwenye begi la kubebea kompyuta mpakato (laptop), lakini
sikuzikuta.
“Niligundua vitu vyangu vingi havipo ndani kama vile
mashati, suruali, redio ndogo na saa ya ukutani. Nilimuuliza mke wangu
akanipa majibu rahisi.
“Nilianza uchunguzi, niliwahoji shambaboi
wangu kuhusu tabia ya mke wangu ambapo waliniambia kila siku nikitoka
kwenda kazini nyuma kuna mtu huingia nyumbani kwangu na kukaa na mke
wangu kwa muda mrefu ndani.
“Kwa kidokezo hicho, siku moja nilichukua
simu ya mke wangu ya kijanjani, nikaipekua na kugundua namba moja
ambayo amekuwa akiwasiliana nayo mara kwa mara. Hii namba aliisevu kwa
jina la Mwajuma Jumanne.
“Ajabu ni kwamba, kwa namba hii nilikuta ujumbe mfupi wa maneno (SMS)
wa mapenzi kati ya mke wangu na huyo Mwajuma Jumanne. Nilianza kuhisi
kuna jambo.
“Moja ya meseji ilisema yeye (Mwajuma) hana mke! Nikajua
huyo Mwajuma ni mwanaume niliyeambiwa na shambaboi kuwa huwa anakuja
nyumbani kwangu.
“Pia upelelezi wangu uligundua kuwa mwanaume huyo ama huwa anamuibia vitu mke wangu au alikuwa anapewa.
“Niliwahi
kuambiwa kuwa kuna siku mke wangu alimpa mwanaume huyo shilingi elfu
sitini (60,000/) na akarudia tena hivi karibuni kumpa kiasi hichohicho,”
alisema kiongozi huyo.
.
Alisema kufuatia mambo yote hayo, aliamua
kwenda Kituo cha Polisi Wazo, Dar kutoa taarifa ya kupotelewa na vitu
akimtaja mwanaume huyo kwamba ndiye anayemtuhumu. Kwa ujasiri mkubwa,
kiongozi huyo aliwaambia polisi kwamba mtu huyo angemtafuta mwenyewe,
likafunguliwa jalada namba WP/RB//7720/2013 WIZI.
Akiendelea kusimulia mkasa huo, kiongozi huyo anasema:
“Siku
ya tukio, nilijifanya nasafiri kwenda Dodoma kikazi ili kumpa mwanya
mgoni wangu kujitawala, niliondoka nyumbani alfajiri huku nikiwa
nimeweka wapelelezi wangu.
“Ilipofika saa tano asubuhi, Hussein aliingia nyumbani kwangu na
kuanza kujimwaga kama kwake bila kujua arobaini yake ilikuwa inatimia
siku hiyo.
“Mimi na wapelelezi wangu tulivamia nyumba, tukagonga mlango, mke wangu akafungua. Aliponiona ni mimi alianguka kwa kiwewe.
“Nilichungulia
ndani kupitia dirishani nikamwona mgoni wangu akivaa shati. Alitoka
mbio kuelekea getini. Nilichomoa bastola na kupiga risasi moja hewani,
ikampagawisha, akataka kupanda ukuta.
“Nilipiga filimbi watu wakaja, walipojua
kisa, walimvua suruali na kuanza kumpa kipigo huku wakimtembeza mpaka
moja ya sehemu anazofanyia biashara zake za kuchemsha supu na kukaanga
chipsi, bahati yake aliokolewa na polisi,” alisema kiongozi huyo.
Alipoulizwa alipo mkewe kwa sasa, alisema: “Nilimtimua mbio, kaondoka zake.”
Alipoulizwa alipo mkewe kwa sasa, alisema: “Nilimtimua mbio, kaondoka zake.”
Kaka wa damu wa Hussein aliyejitambulisha kwa
jina la Tambwe alisema kitendo alichokifanya mdogo wake ni cha aibu ila
anapinga adhabu aliyopewa ya kutembezwa uchi.
“Hili tukio alilofanya
mdogo wangu ni baya, hata baba yetu mdogo hapa mjini siwezi kumwambia
kwa sababu linaweza kumpa presha,” alisema mtu huyo ambaye alimuwekea
dhamana polisi mgoni huyo.
Kaka mwingine wa mtuhumiwa, Hamis alisema mama yao mzazi (hakumtaja
jina) na bibi yao waliopo Tabora walizimia baada ya kusikia tukio hilo
na wameongea kwa simu na mtendewa ili amsamehe mgoni wake.
Mke
wa mtuhumiwa, Pili Muhammed akizungumzia fumanizi la mumewe kwa njia ya
simu akiwa Rufiji, Pwani alisema: “Mume wangu si mkweli katika mapenzi
yetu tangu siku nyingi ila niliamua kuvumilia nikiamini atabadilika
lakini badala yake sasa amekamatwa ugoni.”
Aliongeza: “Siku ya tukio mtoto wetu mchanga alikuwa anaumwa,
nilipomuomba mume wangu anisindikize hospitali aliniambia hajisikii
vizuri, akabaki nyumbani kulinda nyumba.
“Niliporudi sikumkuta na
mpaka giza linaingia hakurejea, baada ya muda kidogo nikaambiwa
amekamatwa ugoni yupo Kituo cha Polisi Tegeta (si Wazo). Ndiyo
nikawapigia simu kaka zake wakaenda kumdhamini.”
Source: Gpl
Source: Gpl