Like Us On Facebook

MFANYABIASHARA AFARIKI GHAFLA NDANI YA DALADALA AKITOKEA BAGAMOYO KWENDA DAR


 
MKAZI wa Mapinga wilayani Bagamoyo, Pwani, Daniel Busianya (58), alindondoka na kufariki alipokuwa amekaa kwenye kiti akisafiri kwenda jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa 3.00 asubuhi maeneo ya Mbuyuni njia panda ya Kunduchi, Kata ya Kilongawima.
 
Kwa mujibu wa Wambura, Busianya ambaye ni mfanyabiashara alikuwa anatokea nyumbani kwake Mapinga Bagamoyo kwenda jijini Dar es Salaam na alipofika Kunduchi ghafla alianguka kwenye kiti alichokuwa amekaa na kufariki papo hapo.
 
Hata hivyo, chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika; maiti imehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari