Wafuasi wa CHADEMA jijini Arusha walioambatana na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli Bw. Amani Salenga wakionyesha bango hilo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani)..
Amani Salenga akiwa na kundi kubwa la vijana walikutana na
waandishi wa habari na kudai kuwa Mbunge wa Arusha, Godbless Lema ndo chanzo
cha vurugu ndani ya CHADEMA kwa kuanzisha kikundi cha vijana
kinachohatarisha maisha ya wale wanaopinga na mawazo ya Lema katika
utendaji wa chama mkoani Arusha.
Amani alisisitiza kuwa kwa kuwa CHADEMA imeamua kufanya maamuzi kwa maslahi ya watu binafsi hususani swala la viongozi waliovuuliwa vyeo vyao(zitto),basi kila mwanachadema anatakiwa atambue kuwa ndani ya chama hicho kuna pande mbili , CHADEMA ASILI na CHADEMA FAMILY.
Vijana hao waliokuwa na mabango mbalimbali wamelaani hatua ya chama chao kuwafukuza viongozi wao pasipokufuata katiba ya chama na kusisitiza kuwa Lema ndo tatizo ndani ya Chadema .