Golikipa Juma Kaseja amesaini Mkataba wa miaka miwili na klabu ya Yanga SC kwa dau la Sh, Milioni 40 mbele ya vigogo wa Usajili wa Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb na Seif Ahmed ‘Magari’ mbele ya Meneja wake, Abdulfatah Salim Saleh Ilala Dar es Salaam.
Kaseja sasa anakwenda kuungana na makipa wawili aliowahi kufanya nao kazi Simba SC, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’
Hii
inakuwa mara ya pili Kaseja kusajiliwa Yanga baada ya awali kusajiliwa
mwaka 2009 akitokea Simba SC ambako baada ya msimu mmoja wa mkataba wake
alirudi Msimbazi.
Kaseja
aliachwa Simba SC mwishoni mwa msimu kwa madai ya kiwango chake kushuka
ambapo kuukosa mzunguko wa kwanza wa Ligi kuu ya bara ingawa sasa
baada ya kumwaga wino Yanga anarudi kazini Januari.
Kikubwa
kilichoisukuma Yanga SC kumsajili kipa huyo ni uzoefu wake katika
michezo ya kimataifa na inataka inufaike naye katika Ligi ya mabingwa
Afrika mwakani.
Kaseja
aliibukia sekondari ya Makongo Dar es Salaam ambako aliitwa timu ya
vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2001 chini ya
kocha Mnigeria Ernest Mokake aliyekuwa akisaidiwa na mzalendo Juma
Matokeyo ambao wote sasa ni marehemu.
Mwaka
huo huo alisajiliwa na Moro United aliyoichezea hadi mwaka 2003
alipohamia Simba alipopiga kazi hadi 2009 akaenda Yanga na kurejea mwaka
mmoja baadaye ambako alifanya kazi hadi mwishoni mwa msimu uliopita
alipotupiwa virago.