Like Us On Facebook

DUDU BAYA AELEZEA HASARA YA WADAIWA KUTOPOKEA SIMU ZA WADENI WAO

Ni mapema sana ila inabidi niiweke kama alivyonisimuliwa mwenyewe Dudu Baya a.k.a Mamba.

Ni hivi, Dudu Baya alikuwa na mdeni wake wa siku nyingi ambaye aligeuka kuwa mdeni sugu hivyo alikuwa anamkwepa kwa kuwa alikuwa anamsumbua mara kwa mara.

Siku moja mwimbaji huyo wa ‘Matope’ alikuwa katika safari zake na gari lake, mara ghafla akafika eneo ambalo kulikuwa kumetokea ajali mbaya ya gari na watu wakawa wanafanya kila njia ili waweze kuwaokoa abiria waliokuwa pale, kwa moyo wa huruma Dudu alijiunga nao katika zoezi hilo.

“Nilipofika pale nikaona mke wa yule jamaa yangu ninaemdai akiwa na mtoto wake wanavuja sana damu masikini, ilinisikitisha sana nikaamua kuwasaidia lakini hali yao ilikuwa mbaya sana.

Sasa nikampigia simu yule jamaa mdeni wangu nimwambie kilichotokea huku, jamaa akanichunia hataki kabisa kupokea simu yangu anadhani nataka kumdai lile deni. Nikapiga simu mara nyingi sana lakini hakupokea.” Ameeleza Dudu Baya.

Dudu amesimulia kuwa baada ya kufanya taratibu zote na kuwafikisha hospitalini, bahati mbaya mke na mtoto wakapoteza maisha. Baadae sana, ndio jamaa akapokea simu aliyopigiwa na Dudu kiasi cha kumaliza chaji ya kimeo cha mtoto wa Mwanza, na alipopokea tu alianza na maneno yanayoashiria kuchoshwa na usumbufu wa Dudu.

Eti baada ya familia yake kupoteza maisha ndo anapokea simu halafu ananimaindi kuwa namsumbua wakati ameshaniahidi tarehe ya kunipa..aah, si ndo nikamwambia tukio lenyewe mara akaanza kulia, na kumbe alikuwa kwenye starehe tu anakula bata.” Ameeleza Dudu.

Tutaimalizia story yote wimbo ukishatoka na video kabisa. Duh, hivi nilikuwa sijasema kama ni wimbo wake unaotarajiwa kutoka mwaka huu mwishoni au mwanzo wa mwaka ujao!

Wimbo unaitwa ‘Pokea Simu’ na umepikwa ndani ya Golf Records ilikofanyika 'Matope'.

Dudu ameiambia tovuti hii exclusively kuwa aliamua kufanya wimbo huu kwa mtindo wa story ya majonzi  ili kutoa fundisho kwa watu wenye tabia za kupotezea simu wanazopigiwa kwa hisia zao binafsi.

-Times Fm
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari