Ukimuona
Timbulo akiwa na baba yake, ni rahisi kuwa na imani kuwa huyo ni babu
yake kutokana na Uzee wake. Ukweli ni kwamba, baba mzazi wa msanii huyo,
ana umri wa miaka 107. Akiongea kwenye kipindi cha Sunrise cha Times
FM, leo, Timbulo alisema wazazi wake wamekuwa wakiugua mara kwa mara
kutokana na umri wao. Katika hatua nyingine, leo ni siku ya kuzaliwa ya
mama yake mzazi, ambaye hata hivyo mama yake huyo hakumbuki mwaka
aliozaliwa. Kupitia
Instagram, Timbulo ameandika: “Kiukweli upendo wako kwangu ni
unreplaceable, cjapata na am sure cwez kupata mwanamke mwenye upendo wa
dhati kama ule unaonipa, furaha na nuru hii hugeuka huzuni na giza kila
nikifikiri cku utakayoniacha ntakuwa katika hali gani, daaaaah mola nipe
la hili swali maana,,,, happy birthday mama yangu mie japo umri na
muonekano wako ni kama bibi yangu na hata umri wako hujui ni miaka
mingapi ila cwez kuubadili ukweli huu ur my mother, am proud of n I love
u so much.”
Source: Times Fm