Marc Jacobs
Mifano
mizuri inaweza kuwa kwa manguli wa fashion duniani kama Valentino
Garavani, Yves Saint Laurent, Perry Ellis, Karl Lagerfeld, Alexander
McQueen, Gianni Versace, Alexander Wang, Giorgio Armani, Marc Jacobs
(Louis Vuitton) Domenico Dolce na Stefano Gabbana, Tom Ford na wengine.
Na hata kwa Tanzania wapo wengi wanaofahamika wazi.
Karl Lagerfeld
Japokuwa
mambo yanabadilika na hasa kwa nchi za wenzetu na kukubalika kwa watu
wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, kumefanya mashoga nao
wafanikiwe kwenye fani zinazotawaliwa na wanaume wa kawaida, lakini
mifano ya dunia halisi inabaki michache na hasa tu kwenye majiji ama
nchi ambazo mashoga na wasagaji wanapewa heshima sawa na wengine.
Pia
kihistoria mashoga kwenye fashion walikuwa wakipewa kipaumbele zaidi
kuliko wanawake. Ni Coco Chanel pekee ndio alikuwa miongoni mwa
wanawake wachache waliofanikiwa kwenye kiwanda hicho kilichokuwa
kikitawaliwa zaidi na mashoga Christian Dior na Cristobal Balenciaga.
Dolce & Gabbana Pili, inasemekana kuwa utamaduni wa ushoga huwapa nafasi watu hao uwezo wa ubunifu. Mashujaa kwenye jumuiya ya mashoga sio wachezaji wa soka ama wanajeshi- japo wapo. Lakini zaidi wapo kwenye muziki, uigizaji, utengezaji wa filamu, uandishi na sanaa zingine. Hii ni kwasababu ya ukweli kwamba hizi ndio zilikuwa kazi ambazo mashoga waliweza kufanikiwa na kuendelea kuwa walivyo na kujivunia wanachokifanya. Uwezo wao wa ubinifu huongezeka na ile sense ya upekee ambayo mashoga huikuza ndani ya ulimwengu wa mapenzi ya jinsia mbili (heterosexual world).
Tom Ford Pointi ya msingi: Upenzi wa mashoga katika urembo, utanashati hauwezi kuelezeka. Inasemekana kuwa mwanaume anayebuni nguo nzuri kwa mwanamke aidha hutaka kuwa na mwanamke ama hutaka kuwa mwanamke’
Credit: Bongo 5

