Like Us On Facebook

BONGO MOVIES WAUKIMBIA MWALIKO WA BUNGE ILI KUSIKILIZA MSWADA WAO

Waigizaji wa filamu nchini wanadaiwa kukwepa mwaliko bungeni walikotakiwa kwenda kutoa muswada wa marekebisho kwenye sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza (1976).
 
Kupitia Twitter muigizaji mrembo, Yobnesh Yussuph maarufu kama Batuli, amesema amefuatilia mjadala huo kupitia TV lakini amesikitishwa kubaini kuwa wapo wasanii walioalikwa lakini hawakwenda bungeni.
 
Yes nimefuatilia bunge ila cha kusikitisha ni wasanii waliopewa mwaliko halafu hawajaudhuria,” aliandika Batulli.
 
Nalaani sana kitendo cha walioalikwa kutokufika bungeni kwenye hoja nyeti kama hii nikiwajua sitawanyamazia,” aliongeza.
 
Naye Lulu alijibu: Hatujichukulii serious ndo mana hatuchukuliwi serious pia..unaachaje kuhudhuria mwaliko unaokuhusu halafu umealikwa? Ndo tatizo la kutokuwa na umoja, haya tutaendelea kulia tu.”

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
 

KILELE CHA HABARI Copyright © 2014 -- Template created by Mbatta -- Powered by Kilelechahabari