MSANII filamu na muziki wa kizazi kipya wa Tanzania Baby Joseph
Madaha maarufu kwa jina la Baby Madaha amesema kwamba msanii mwenzake wa
muziki nchini,Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platinumz si
msanii bali ni mfanyabiashara ya ngono.
Madaha amesema kwamba Diamond si mwanamuziki na kwamwe huwezi
kumlinganisha na msanii kama Barnaba Boy, anayefanya muziki kama sanaa
na kazi kulingana na kipaji chake na kwamba Diamond si msanii wa muziki
bali ni msanii ngono anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.
“Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapo jitambua na
kuacha kulewa penzi la Diamond ndiyo itakayokuwa mwisho wa maisha yake
kimuziki,kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaanza
kuporomoka”alifafanua Baby Madaha