HABARI
YA KUSIKITISHA: KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili wenye
umri wa miaka saba na nane wametelekezwa na wazazi wao kwa muda wa miezi
mitano bila huduma za msingi. jijini Mbeya
Agustino Steven (8) akiandaa ugali ale na dada yake
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakichambua mboga aina ya mchicha |
Mwenyekiti
wa Dawati la Jinsia chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo amesema
baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji watoto
hao ambapo pia aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia jeshi la
Polisi ili kuwabaini wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za
kisheria.
|
Agustino Steven (8) akipika mchicha |
Hii ndiyo sahani yao wanayotumia kwa ajili ya chakula |
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) hapa wakila chakula walichopika wenyewe |
Unga pamoja na maharage |
Hili ndilo sanduku lao |
Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) wakiwa nje ya nyumba wanayoishi
KATIKA
hali isiyokuwa ya kawaida watoto wawili wenye umri wa miaka saba na
nane wametelekezwa na wazazi wao kwa muda wa miezi matano bila huduma za
msingi.
Watoto hao wamefahamika kwa majina ya Agustino Steven (8) na Rebeka Steven(7) ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mapambano iliyopo Kata ya Iyela Jijini Mbeya.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti watoto hao wamesema Wazazi wao waliwaacha kwenye
nyumba ya kupanga tangu mwezi wa Mei mwaka huu ambapo Baba inasadikika
alielekea Umalila Mbeya Vijijini ambako inasemekana ameoa mke mwingine.
Wamesema
Mama yao alielekea Mbozi ambako pia naye inasadikika ameolewa na
mwanaume mwingine hivyo kuwaacha watoto bila kuwa na huduma za msingi
kama Chakula na mavazi huku wakiwa wameachiwa Nyumba mtaa wa Jakaranda Airport.
Aidha
watoto hao waligundulika baada ya kukutwa mitaani wakitafuta riziki
kwa kuzoa taka kwenye majumba ya watu kisha kupeleka majalalani kwa
ujira wa kati ya shilingi 200 na 500 ambazo huzitumia kununua mahitaji ya nyumbani pamoja na kujipikia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Dawati
la Jinsia chini ya Jeshi la Polisi, Mary Gumbo amesema baada ya kupata
taarifa hizo alifika eneo la tukio na kuwahoji watoto hao ambapo pia
aliwaomba majirani na wananchi kulisaidia jeshi la Polisi ili kuwabaini
wazazi walipo ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Amesema
majirani pia waendelee kuwa karibu na watoto hao hadi pale wazazi wao
watakapopatikana kwa kuwahudumia na kuhakikisha wanaendelea na masomo
kama kawaida.
Amesema
kitendo kilichofanywa na wazazi hao ni cha kinyama hivyo wakipatikana
hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ambapo pia alitoa wito kwa jamii
kuacha vitendo vya kikatili.
Kutokana
na ugumu wa maisha binti huyo katika harakati za kutafuta chochote kwa
ajili ya wadogo zake ameishia kuzalishwa mtoto wa kiume ambaye ana
mwezi mmoja sasa na kuwakimbia wadogo zake nay eye kukimbilia kwa
rafiki yake.
Pia
Jeshi la Polisi kupitia dawati la Jinsia limeamua kulifuatilia suala
hilo kwa kumtafuta kijana aliyemzalisha binti huyo aliyefahamika kwa
jina moja la Hezron ambaye imedaiwa kuwa walikuwa wakikutana kwenye
nyumba ya kulala wageni(Gesti ).
|